Mrembo wa mavazi wa Malaysia ambaye alihukumiwa mwezi uliopita kuchapwa bakora baada ya kukamatwa akinywa pombe kwenye kumbi ya starehe atachapwa bakora sita wiki hii. Mahakama ya kiislamu nchini Malaysia ilitoa hukumu mwezi uliopita ikiamuru mrembo wa vivazi Kartika Sari Dewi Shukarno, 32, achapwe bakora sita baada ya kukamatwa mwaka jana akinywa pombe katika klabu ya starehe katika jimbo la Pahang mashariki mwa nchi hiyo. Mwendesha mashtaka Saiful Idham Sahimi alisema kwamba Kartika atakuwa mwanamke wa kwanza kuchapwa bakora kwa kunywa pombe chini ya sheria ya kiislamu kwa kuwa ameamua kutokata rufaa hukumu hiyo aliyopewa. "Hii ni mara ya kwanza nchini Malaysia.. ni adhabu nzuri kwasababu katika sheria za kiislamu mtu anayekunywa pombe anafanya kosa kubwa sana" alisema. Katrika ataendelea kuwa mahabusu hadi hukumu yake ya kuchapwa bakora itakapotelekezwa na ataachiwa huru muda mfupi baada ya hukumu hiyo. Saiful alisema kwamba bakora zitakazotumika katika kumchapa Katrika ni nyepesi sio kama zile zinazotumika kuwachapa wanaume.
Saiful alisema kwamba adhabu hiyo ina lengo la kuelimisha zaidi sio kuwaumiza watu. Theluthi mbili ya watu wa Malaysia ni waislamu na hukumu zao kuhusiana na makosa yote ya kuvunja sheria za nchi pamoja na ya kidini hutolewa na mahakama za kiislamu. Kwa wale ambao si waislamu huruhusiwa kunywa pombe wakati wowote na mahakama za serikali hutumika kutoa hukumu katika makosa yao mbali mbali ya kuvunja sheria za nchi. Mahakama za serikali nazo hutoa adhabu ya bakora kwa watu wanaopatikana na hatia za makosa ya ubakaji na rushwa. Kartika alisema kwamba alitaka mamlaka husika zitekeleze adhabu hiyo mapema iwezekanvyo ili aweze kuendelea na maisha yake pamoja na mumewe na wanae.
Klabu za starehe za Malaysia huuza pombe kwa watu wote bila kuangalia kama wewe ni muislamu au sio muislamu, ni jukumu la waislamu kujiangalia wenyewe wasivunje sheria kwa kununua na kunywa pombe.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Thursday, August 20, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment