Mwangalie vyema.. Wenzake wanalalamika kuwa huyu mkaka sio mdada. Mwanariadha wa kike wa wa Afrika Kusini wa mbio za mita 800 ameponzwa na mwili wake wenye misuli iliyojengeka kama mwanaume kiasi cha kuwatia hofu wanariadha wenzake wa kike na kusababisha shirikisho la riadha duniani liamue achunguzwe kama kweli ni mwanamke.Nyota wa riadha wa Afrika Kusini wa mbio za mita 800 za wanawake, kutokana na kuwa na misuli iliyojengeka kama mwanaume na uwezo wake mkubwa katika mbio hizo anafanyiwa uchunguzi wa jinsia yake kuthibitisha kuwa kweli ni mwanamke.Tumbo lililokata miraba minne, vinyweleo vyake vya usoni na mwili wenye misuli iliyojengeka kama anavyoonekana kwenye picha hizo, imesababisha mwanariadha wa kike wa Afrika Kusini, Caster Semenya kutakiwa kufanyiwa vipimo vya kuthibitisha jinsia yake.Shirikisho la kimataifa la riadha duniani (IAAF) limesema kwamba lilitaka Semenya afanyiwe vipimo hivyo wiki tatu zilizopita ili kumwezesha kushiriki kama mwanamke kwenye mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea Berlin, Ujerumani.Shirikisho la riadha la Afrika Kusini lilisema kwamba lina uhakika wa asilimia mia moja kwamba Semanya mwenye umri wa miaka 18 ni mwanamke."Tusingemwingiza kwenye mbio za wanawake kama tungekuwa na shaka yoyote kuhusiana na jinsia yake" ilisema taarifa ya shirikisho hilo.Semenya anaiwakilisha Afrika Kusini kwenye mbio hizi akiwa amejijengea jina baada ya kuwa bingwa wa mbio hizo wa Afrika.Semenya ndiye anayetabiriwa kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 800 za wanawake kwenye fainali ya mbio hizo nchini Ujerumani. Tusubiri vipimo...
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment