Zombe Akiingizwa mahakamani wakati wa siku za mwisho za kufuatilia mwenendo wa kesi.Kamanda wa zamani wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe ameachiwa huru leo na mahakama kuu katika kesi iliyomuhusisha na tuhuma za kuwaua wafanyabiashara hao wa madini ya rubi na dereva teksi. Jaji Salum Masatti ndiye aliyetoa hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa baada ya vuta nikuvuta ya kisheria ya mwaka mmoja baina ya mawakili wa pande zote mbili, tangu kesi hiyo ilipoanza rasmi kusikilizwa Mei 28, 2008. Zombe na wenzake walituhumiwa kuwaua kwa kukusudia Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na Mathias Lunkombe ambao ni wafanyabiashara wa Mahenge. Mwingine ni dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu. Inadaiwa kuwa watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye msitu wa Pande ulioko Mbezi Luisi wilayani Kinondoni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Watu hao walikamatwa na polisi kwa madai ya kuhusika kwenye tukio la ujambazi jijini Dar es salaam, lakini gazeti hili likaripoti baadaye kuwa waliouawa hawakuwa majambazi baada ya kuzungumza na watu wa sehemu mbalimbali, zikiwemo Mahenge na Sinza. Taarifa hiyo ilisababisha Rais Jakaya Kikwete kuunda tume iliyoongozwa na Jaji Kipenka Mussa ambayo uchunguzi wake ulisababisha kutiwa hatiani kwa watu hao na kufunguliwa kesi.Hukumu ya leo ya Jaji Masatti imepokewa kwa hisia tofauti na bila shaka kicheko na kilio vilikuwepo.
Ilikuwa mshike mshike mahakamani pale zombe alipotoka mlango wa nyuma wa mahakama na kufanyashughuli za upigaji picha ziwe ngumu(Pcha kwa hisani kubwa ya Michuzi Sn. na vyanzo vingine)
Amka Na BBC
43 minutes ago
0 comments:
Post a Comment