Hebu fikiria umo ndani ya ndege halafu unapata taarifa kuwa marubani wote wamepitiwa na usingizi ...na ndege wanayoiongoza ikapita kwenye uwanja wa ndege huku wao wakikoroma?Rubani na msaidizi wake wa ndege ya shirika la ndege la Go! Airlines waliuchapa usingizi wakati ndege ikiwa angani wakati wakikaribia kufika uwanja wa ndege ambao ndege hiyo ilitakiwa kutua.Abiria 43 wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea kwenye kisiwa cha Hawaii kutoka kwenye kisiwa kingine cha Honululu, walibaki wamepigwa na butwaa wasielewe kinachoendelea walipochungulia madirishani na kuona wameupita uwanja wa ndege kwa juu na wameanza kuchanja mbuga kukatiza baharini.Rubani huyo na msaidizi wake walizinduka kutoka usingizini baada ya kuamshwa na waongoza ndege kwenye uwanja wa ndege wa Hilo International ambao ndege hiyo ilitakiwa kutua.Wakati huo ndege hiyo ilikuwa futi 21,000 toka ardhini na ilikuwa imeshatambaa kilomita 48 kutoka kwenye uwanja wa ndege huo.Baada ya kuzinduka marubani hao waliigeuza ndege hiyo na kutua salama kwenye uwanja huo. Matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo lililotokea mwezi februari mwaka jana, yametolewa wiki hii na bodi ya usalama katika usafirishaji (NTSB) ambayo imethibitisha kwamba marubani hao walilala kutokana na uchovu wa kazi.NTSB ilisema kwamba marubani hao walifululiza siku tatu wakiendesha ndege asubuhi kuanzia saa 11 alfajiri.NTSB pia ilisema kwamba mbali na uchovu wa kazi, rubani wa ndege hiyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa usingizi wa Apnea ambao ulimsababishia awe anasinzia sana nyakati za asubuhi na mchana.haya sasa ..gari linapanda mlima kitonga dereva kapitiwa itakuwaje?
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, August 18, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment