Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, August 10, 2009


kimbunga kilichopiga pwani ya magharibi mwa Japani kimesababisha mvua kubwa na baadaye mafuriko na maporomoko ya udongo na huku kukiwa na taarifa ya watu kumi na wawili kupoteza maisha na watu wengine 10 hawajulikani waliko hivi sasa na jitihada zinaendelea za kuwasaka.
Kimbunga hicho kiitwacho Etau kimetokea katika mkoa wa Hyogo kama kilometa 500 hivi magharibi mwa Tokyo. Afisa Polisi mmoja aliyejulikana kwa jina la Shigekazu Kamenobu amesema kuwa kwa sasa hawezi kueleza madhara kamili juu ya kimbunga hicho lakini tukio la karibuni lililothibitishwa ni kuwa mtu mmoja alisombwa na maji akiwa anaendesha gari lake na mwili wake ulipatikana baadaye ukiwa ndani ya gari lake.
Polisi wanasema kuwa takriban watu 2,200 walihamishwa kutoka katika makazi yao huko Hyogo na kwa sasa wanaishi katika majengo ya umma ikiwa ni pamoja na majengo ya shule na nyumba 500 zinatajwa kuwa zimesombwa na maji.
Shirika la Utabiri wa hali ya hewa ya Japani limeonya kuwa kuna uwezekano wa kutokea mvua kubwa na maporomoko ya udongo mashariki mwa Japani itakayotokana na kimbunga hicho.

0 comments: