Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, August 10, 2009



Jana Alhamisi asubuhi tetemeko lilitikisa jiji la Tokyo kwa sekunde kadhaa lakini bado haijajulikana kama limeleta madhara...Lakini habari za kuaminika ni kuwa wadau wote kutoka Tz wapo safi..Jumapili iliyopita saa moja na dakika 56 , tetemeko lenye ukubwa wa 6.9 kipimo cha richa lilitetemesha katikati ya Japani na eneo la Kaskazini. Sote tulikuwa tukipata hekaheka huku tukifuatilia matangazo baada ya tukio hilo ambapo wataalamu wanasema kiini cha tetemeko hilo kilikuwa kusini mwa Tokyo katika bahari ya Pacifiki km 211 chini ya bahari lakini kimbembe chake kwa watu wa juu huku balaa!Shirika la utabiri wa hali ya hewa linasema kuwa hakuna madhara yaliyoripotiwa ingawa treni zilizokuwa safarini zilisimama kwa muda hadi kulipotulia shughuli ziliendelea kama kawaida.du inataka moyo!

0 comments: