Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, August 22, 2009

Huu ni msikiti wa madina wakati ambapo hakuna pilikapilika za hijja. Waislamu nchini Japani wameanza kufunga kama ilivyo kwa waislamu wengine kote ulimwenguni.Tangazo limetolewa kwa waislamu waliopo Japani huduma ya futari na daku itakuwepo katika mgahawa uliopo karibu na Club ya zamani ya Masaya iliyopo iliyopo Odakyu Sagamihara .Chakula kitaandaliwa na Ma-cheff waliobobea Bi. Tatu Bwela na Sabina Itambiko. Kwa mujibu wa waandaazi vyakula vitakavyohudumiwa ni pamoja na FUTARI-Muhogo wa nazi na samaki,nyama ya mbuzi,kuku,muhogo wa nazi(sukari) ,viazi vitamu, tambi za nazi za kukaanga,--Maandazi ya maua,vibibi, vipopo,tende halua.-Viazi mviringo na nyama ya kusaga na uji wa pilipili.Kwa mkazi wa Japani anaweza kuwasiliana na wahusika kwa simu ya viganjani kupata ramani na utaratibu. Kila la Kheri.
-

0 comments: