WANAWAKE wawili wanashikiliwa na polisi kwa kudaiwa kujihusisha na uuzaji wa vipodozi vya kuongeza maumbile huko maeneo ya Kariakoo jijini Dar.
Watuhumiwa hao majina yao hayakupatikana mapema kwa sababu za kiupelelezi walikamatwa katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wakiuza vipodozi hivyo kwa siri.Watuhumiwa hao walidaiwa kujihusisha na kuuza vipodozi vinavyosababisha kuongeza maumbile ya akina mama maeneo ya makalio na matiti ambavyo vinapigwa marufuku na Serikali visitumike nchini.Hivyo ilidaiwa kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wanatoa vipodozi hivyo nchini China kwa lengo la kuwauzia akina dada wenye malengo ya kuongeza makalio na matiti vikiwemo na vipodozi vya kubana maumbile sehemu nyeti kwa akina dada kurudisha bikira.Vipodozi hivyo viligundulika hivi karibuni vikitumika na wakinadada wengi na serikali kupiga marufuku uingizaji na uuzaji wa vipodozi hivyo nchini.Serikali ilipiga marufuku uingizaji wa vipodozi hivyo na wafanyabiashara wa vipodozi hivyo wanaendelea kuuza kwa njia ya siri madukani.Hivyo Mamlaka ya Chakula na Dawa wapo kwenye operesheni endelevu na kuzunguka maeneo ya jiji kuwakamata wanaoendelea kuuza vipodozi hivyo na kuwachukulia hatua za kisheria.Awali serikali ilikataza uingizaji wa vipodozi hivyo na kupiga marufuku kutumia vipodozi hivyo kwa kuwa utafiti uliofanyika uligundua kuwa vipodozi hivyo vina madhara kwa watumiaji na kumsababishia mtumiaji wa vipodozi hivyo baadae kuathirika na magonjwa ya kansa.Wafanyabishara hao walifkishwa katika kituo cha Msimbazi Polisi huku upelelezi wa kina ukiendelea....Duh...Haya mwanadada nawe wasemaje..!
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, August 14, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment