Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, September 01, 2009

Shinjuku jijini Tokyo , Bustani ya kupendeza . Yalikuwa mapumziko mazuri ya mchana mie -BM na Komredi Reginald Ndesika katika eneo hilo.Safii mno!
Bustani hii iko magharibi mwa Shinjuku maarufu kwa jina la Shinjuku Central Park, eneo dogo lililotunzwa vizuri likiwa na miti na bustani kijani kiwiti na maji yalitiririka juu ya mwamba …mmh sijui origino au mwamba umepandikizwa…lakini inapendezaBustani hii iko karibu na majengo marefu zaidi nchini Japani ikiwa ni pamoja la la jengo la serikali linalofahamika hapa Japani Tokyo Metropolitan Government Twin Buildings. Picha hii imepigwa kutoka juu eneo la Shinjuku kuionyesha bustani hii. Inafurahisha kuona bustani zilizotulia katikati ya majiji makubwa kama Tokyo. Ningeweza niicopy na kupesti pale Kariakoo. ...Du! Hebu hapo...kumbukumbu.
Mkuu alikula pozi hapo..imetulia naona.
Wacha niweke sawa kitendea kazi tuingie dukani..Na hapo..Ziara yetu ilitufikisha kwenye moja ya maduka maarufu nchini Japani la vifaa vya elektroniki hususan Camera eneo la Shinjuku :BIC CAMERA: pamoja na yote tulivutiwa na kifaa cha kamera ambacho kinakuwezesha kupiga picha katika masafa marefu ..Kuchungulia ruhsa. href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjx-ghnDqPh_iTOsevAosABVez_Foyv-10Pbio8zztgb8OPWjh5U4SL8LFmR9yZ3uXk1ynBjIkLXHua_U33frVkrENWXHu9Ra5tqVhyphenhyphen2IyNqeysLdbe3BnIcTkJFOlLz0n3xoQPrrURz-Y/s1600-h/Falls+006.jpg"> Komred Ndesika alianza kuhakiki...mmmh!
Aaah Kweli...nimeona!
Kunako chombo twarejea tulikotoka..

0 comments: