Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, September 12, 2009


Kijiji cha Lusanga kipo wilayani Mvomero mkoani Morogoro. Ni kijiji chenye historia ndefu na kimekuwepo hapo miaka mingi iliyopita. Moja ya sifa za kijiji hicho ni ardhi iliyo na rutuba. Mazingira asili hayajaharibiwa hata chembe . Mgosi Peter Omari alikuwa hapo na akafyotoa picha na kuzimuvuzisha kwenye Mirindimo. ...Nimewakumbuka ze Comedy!

Virgin Land; Kiswahili chake Kiguumu.Oke... Hapajalimwa hapo tangu paumbe....au!

Wazee wanatuambia minazi hiyo imekuwepo kwa miongo mitano sasa , miaka 50. Lakini hadi leo madafu, nazi na pombe ya mnazi inapatikana kwenye minazi hiyo hapo Lusanga.

Miti asili kama hii imetapakaa katika kijiji hicho na kutengeneza mandhali ya kipekee

Ubunifu wa watoto wa Lusanga.

0 comments: