Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, September 12, 2009


Safari kuelekea nyumbani kwa Mwenyekiti wa Tanzanite , Japani lazima ufike hapa Kunitachi.Naelekea huko sasa nina mwaliko..

Lango la kusini la kituo cha treni cha Kunitachi, nimekutana na teksi zikiwa katika foleni ya kistaarabu....Inapendeza.

Mwenyekiti wa Jumuia ya watanzania wanaoishi Japani inayojulikana kama Tanzanite alipata wageni nyumbani kwake kufuatia mwaliko wake alioutoa kwa ajili ya Futari.
Kati ya waalikwa mashuhuri ni ni Mr. Tutuba na Mr. Herman Mpangile wakiwa katika vyuo vikuu hapa Japani kuongeza maarifa. nami nilialikwa . Pamoja na futari nilipata kusikiliza busara ya viongozi wetu. Ilikuwa hafla ya kufana iliyoandaliwa na Dr. Simba na Mkewe Fatma. Pitisha macho. Hapo menyu ya leo ya Futari , Nyumbani kwa Mwenyekiti.

Mama mwenye Nyumba ndiye aliyefanikisha haya yote..take 5 Mrs. F.Simba
Mwenyeji wetu Dr.Ally Simba Akiwa nasi katika risq iftar.

Wageni waalikwa:Kutoka kushoto Bm, Tutuba na Herman Mpangile . Wakubwa wananoa vichwa katika Vyuo vikuu hapa japani..lakini leo pamoja nao tulikuwa tukifutariswa kwa Mwenyekiti.

Raha ya funga ...futuru Hongereni Mr.and Mrs. Simba.

1 comments:

mumyhery said...

mwanangu unafuturisha umesahau hijabu