Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, September 09, 2009

Wakuu wa nchi na viongozi waandamizi wa Serikali katika picha tya pamoja mwanzoni mwa mkutano wao wa Sadc huko Kinshasa juzi jumatatu.Kutoka kushoto kwenda kulia , waziri mkuu wa Angola Paulo Kassoma, Waziri Mkuu wa Lesotho Pakalitha Mosisili, Raisi wa Botswana Ian Khama, Mfalme Mswati III wa Swaziland, Katibu mkuu wa SADC Tomaz Augusto Salomao, Raisi wa DRC Joseph Kabila, Raisi wa Afrika kusini Jacob Zuma, Raisi wa Msumbiji Armando Emilo na Raisi wa Zimbabwe, Komred Robert Mugabe . Wakati huo Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai alikuwa hajafika.
Majukumu!...Mwenyekiti wa “ Southern African Development Community kwa kifupi (SADC) “ anaeyemaliza muda wake Raisi Jacob Zuma wa Afrika Kusini akimkabidhi jukumu hilo Raisi wa Democratic Republic of Congo (DRC) Joseph Kabila katika Mkutano wao ulioanza juzi jumatatu huko Kinshasa, DRC Sept. 7, 2009. Katika hotuba aliyoitoa katika mkutano huo Bw. Kabila alisema kuwa amani imeanza kurejea DRCjambo lililowezesha mkutano huo wa 29 wa SADC kufanyika. Mkutano huo uliomalizika jana Jumanne ulifanyika katika ikulu ya Raisi mji unaojulikana kama Umoja wa Afrika eneo la Ngaliema nje kidogo ya inshasa ambako mtawala aliyepita Mobutu Sese Seko alijenga Ikulu yake ya kifahari. Mikutano kama hii imefanyika nchini huo katika miakaya 80 na hata baadhi ya Maraisi wa nachama wa SADC walikanyaga DRC kwa mara ya kwanza ikiwa ni pamoja na Jacob Zuma, King Mswati III Armando Guebuza, Festus Mogae of Botswana na Raisi Rupiah Banda wa Zambia.
Mugabe....
Mmoja wa Viongozi aliye kaa madarakani muda mrefu zaidi Ulimwenguni na aliye na umri mkubwa Robert Mugabe akiwa kikaoni.
Wazimbabwe...
Huku hayo yakifanyika huko DRC ubalozi wa Zimbabwe huko London ulivamiwa na waandamanaji wakidai kuna ukiukwaji wa haki za binaadamu nchini mwao . …zali.

0 comments: