Paparazi aliyejizolea umaarufu kwa kujitosa.Mwandishi wa habari mwanamke wa Sudan aliyepatikana na hatia ya kuvaa suruali na kuhukumiwa kifungo cha mwezi mmoja, ameachiwa huru baada ya kukaa jela siku moja tu.Lubna Ahmed Hussein alipelekwa gerezani baada ya kukataa kulipa faini ya kiasi cha dola 200 za Marekani akisema asingependa ''kuihalalisha hukumu aliyopewa''. Mohedinne Titawi, wa chama cha waandishi wa habari nchini Sudan, amesema chama hicho kimelipa faini ili mwanamama huyo aachiliwe huru lakini yeye akaomba fedha hizo zirudishwe ili aone hatima ya shauri lake.. Hata hivyo Chama cha waandishi wa habari nchini humo kiliwasilisha dola mia mbili za Kimarekani Mahakamani na hivyo Mahakama ikaamuru aachiwe huru. Bi Hussein, alikuwa akikabiliwa na hukumu ya kuchapwa viboko hadi 40. Vikundi vya kimataifa vya kutetea haki za binadamu vilikuwa vikishutumu kesi hiyo tangu ilipoanza, huku Umoja wa Mataifa ukisema siku ya Jumanne kwamba mashtaka dhidi ya mwanamama huyo yalikuwa ni kinyume na sheria za kimataifa. Mwanamama huyu aliwahi kuwa Afisa wa habari wa Umoja wa Mataifa lakini ameacha kazi hivi sasa. Tayari Raisi wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amemualika katika Ikulu ya Parisi kukutananaye ana kwa ana. Akiingia mahakamani na kivazi chake kilichomponza!
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment