Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, September 11, 2009


Mtoto wa miaka nane anayesoma shule ya msingi Shiba-minami elementary katika jiji la Kawaguchi hapa Japani amefariki jana Alhamisi baada ya kuanguka kutoka kikorido cha ghorofa ya nne cha shule hiyo hadi chini ya jengo karibu mita 12. Baada ya tukio hilo la kusikitisha Mtoto huyo alikimbizwa hospitalini lakini saa nne baadaye alifariki dunia. Kwa mujibu wa Polisi tukio hilo limetokea saa tisa na nusu za jioni na inasemekana hakukuwa na wanafunzi wala wafanyakazi shuleni hapo alipokutwa na maafa hayo . Inasemekana wazazi wake walimfuata mtoto wao hapo shuleni na walimuona wakati anaanguka kutoka ghorofani.Picha inayowaonyesha watoto wakitoka shuleni haina uhusiano na motto aliyefariki ingawa furaha ya watoto wakimaliza siku shuleni huenda marehemu angekuwa nayo kama angekuwa hai.

0 comments: