Marekani ina mpango wa kupeleka chombo chake angani ambacho kitaupiga mabomu mwezi ikiwa ni mojawapo ya hatua ya utafiti unaoendelea wa kugundua kama kuna maji kwenye mwezi. Shirika la utafiti wa anga la Marekani (NASA) linajiandaa kuzindua mpango wake unaoitwa LCROSS (Lunar CRater Observing and Sensing Satellite) ambapo mwezi utapigwa mabomu katika harakati za NASA kugundua kama kuna maji angani. Katika mpango huo kombora linaloitwa Centaur ambalo linaenda spidi mara mbili ya spidi ya risasi litatumika kuulipua mwezi ili kutengeneza shimo kwenye mwezi.
Wanasayansi wa NASA wanasema kwamba mlipuko utakaotokea utakuwa mkubwa sana kiasi cha kwamba vipande vikubwa vya vifusi toka kwenye ardhi ya mwezi vitaweza kuonekana kutokea duniani kwa kutumia darubini kubwa.Mabomu hayo yamepangwa kulipuliwa kwenye mhimili wa kusini wa mwezi ambako wanasayansi wanaamini mabilioni ya barafu zilizoganda yanapatikana mita kadhaa chini ya ardhi ya mwezi.Chembe chembe za vumbi la mwezi zitafanyiwa uchunguzi ili kugundua kama kuna dalili ya kuwepo kwa maji yaliyoganda au mvuke.Kugundulika kwa maji kwenye mwezi kutasaidia sana safari za baadae za utafiti wa anga."Kusafirisha maji na vifaa vingine kutoka duniani hadi kwenye uso wa mwezi ni gharama sana" NASA lilisema na kuongeza "Kupatikana kwa maji au barafu kwenye mwezi kutasaidia kupunguza gharama za safari za kwenda mwezini".Chini ni Video inayoonyesha jinsi mwezi utakavyolipuliwa
DKT. NCHEMBA AKARIBISHA SAUDI ARABIA KUWEKEZA TANZANIA
32 minutes ago
0 comments:
Post a Comment