Kabla ya kusoma habari hiyo kwa kina , kwanza burudisha macho kwa Picha za Raisi Barack Obama akiwa katika matukio tofauti.
Rais wa Marekani, Barack Obama, ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2009.Kamati kuu wa tuzo ya Nobel imesema kiongozi huyo ameshinda tuzo hiyo kutokana na juhudi zake kuimarisha uhusiano mwema kati ya watu wa dunia. Kamati hiyo ilitaja moja wapo wa juhudi za Obama katika kuunga mkono mashirika ya dunia kuafikia kuwepo na ulimwengu bila silaha. Msemaji wa Bw Obama amesema rais huyo amepokea taarifa hiyo kwa unyeyekevu. Msemaji huyo alimuamsha rais Obama punde tu habari hizo kutangazwa. Jumla ya watu 205 waliteuliwa kupata tuzo hiyo, akiwemo Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na mwanaharakati wa mageuzi nchini Uchina Hu Jia. Mshindi wa tuzo ya Nobel hupokea medali ya dhahabu, cheti cha diploma na dola milioni 1.4.Tangu kuchukua hatamu za uongozi rais Obama amesimamia masuala muhimu ya dunia ukiwemo mpango wa amani Mashariki ya Kati na kutoa nafasi ya mazungumzo kuhusu mpango wa Iran wa nuklia. Baadhi yawatu hususan wanasiasa wanahoji uamuzi wa kamati hiyo ya Nobel kuwa Obama hakustahili kwakuwa ameonyesha nia na hakuna vitendo ambavyo tayari vinaonekana vya upatikanaji wa amani duniani. Lakini Ukweli unabaki kuwa nadharia na dhamira ya dhati ya Kiongozi wa taifa kama Marekani ni muhimu kubadili mitazamo ya dunia iliyokatika uhasama na vurugu kubwa za kivita.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, October 10, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment