Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, October 08, 2009

BOFYA HAPO: Utapata taarifa ya kina kwa njia ya video juu ya Kimbunga cha Jana Alhamisi kilichotokea hapa Japani kutoka BBC. Kimbunga cha Melor kimepita katika maeneo mengi nchini Japani leo Alhamisi na kupoteza maisha ya watu watatu na wengine 56 wakiachwa na majeraha. Kimbunga kinachofanana na hiki kilitokea miaka miwili iliyopita lakini kile kinachokumbukwa zaidi ni cha mwaka 2004 kilichopoteza maisha ya watu 95. Hali ya leo imevuruga ratiba za ndege , reli na barabara.
Kimbunga kilianza katika mkoa wa Aichi katika rasi ya Chita alfajiri saa 11 na kuvuma kuelekea Kaskazini mashariki kuhu kasi yake ikipungua taratibu nah ii ni kwa mujibu wa Shirika l Utabiri wa hali ya hewa ya japani. Huko Minabe, Mkoa wa Wakayama Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Hiroshi Kitahara mwenye miaka 54 alipoteza maisha baada ya kuzidiwa na upepo alipokuwa juu ya baiskeli yake akisambaza magazeti asubuhi subuhi kazi zinazofanywa sana hapa Japani katika jitihada za kuharakisha habari kwa wananchi. Hiroshi alijikuta ghafla akiparamia mti ulioangushwa na upepo mbele yake kifo ambacho kinafanana na kile kilichomkuta Masaichi Kaji, 69 ambaye alipigwa na tawi la mti kichwani akiwa karibu na hekalu huko Fujimi mkoa wa Saitama dhahiri ikiwa ni kujisalimisha katika eneo takatifu.Zaidi ya safari 440 za ndege za ndani na za kimataifa zilisimamishwa na hata treni ziendazo kasi pia zilisimama kwa muda hapa Japani kupisha kimbembe cha kimbunga. Shule zote za msingi na sekondari za chini jijini Tokyo hasa za kwenda na kurudi nyumbani zilisitisha masomo leo.
Taarifa za uhakika zinabainisha kuwa hakuna raia wa Tanzania au nchi nyingine barani Afrika alipoteza maisha wala kujeruhiwa. Mwandishi wa habari hizi alisafiri mapema asubuhi katika treni kuelekea Shibuya , katikati ya Tokyo saa mbili asubuhi katika treni iliyojaa pomoni kuwahi makazini na hali ya taharuki ilionekana nyusoni mwa watu. Hata hivyo ilionekana dhahiri kuwa watu watu walikuwa nahabari za kutosha juu ya tukio hilo na jinsi ya kujikinga na madhara.

0 comments: