Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, October 08, 2009



Wajapani leo wako kwenye hali ya hadhari kufuatia uwezekano usio na shaka wa kutokea kimbunga kiitwacho Melor katika maeneo mengi ya kisiwa hicho. Inatajwa kuwa kimbunga hicho ni kikubwa kupata kutokea katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na kwamba kitaambatana na mvua kubwa itakayosababisha uharibu mkubwa na bila shaka kutatiza usafiri.
Tayari rasharasha zimejitokeza huk Amami-Oshima , Okinawa ambapo nyumba 1500 zimeachwa bila umeme kutokana na kunusa kwa kimbunga hicho kilichoambatana na etemeko la ardhi. Mashirika ya ndege yamesitisha Safari za ndani takriban 150 ili kukwepa balaa hilo.
Kwa kifupi wastani wa kasi ya upepo inatarajiwa kufikia km 153 kwa saa na hii inakumbusha mwaka 2004 ambapo kimbunga kama hiki kilitokea na kupoteza maisha ya watu 95.

0 comments: