Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, December 13, 2009


Moja ya vikorombwezo vya jiji la Mwanza , ukiona picha hiyo tu unaweza kusweka matonge bila shida. Hongereni kwa ubunifu; wale walobuni hii!
Hapa jana jijini Mwanza palikuwa hapatoshi, Chuo cha Biashara CBE , kulikuwa na mahafali na watu walipata nondos zao, Hongereni sana .Walo mbali na wa karibuni fuatilieni tukio hilo kwa njia ya picha. Mgeni rasmi katika mahafali hayo ,Naibu waziri wa biashara na masoko Mh. Cyril Chami akiwahutubia wahitimu na waalikwa. Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kupewa vyeti vyao. MC alikuwa mtangazaji wa siku nyingi wa Star TV na Redio Free Africa, Bi. Joan Itanisa ambaye sasa ni mhadhiri msaidizi St. Augustine University. Take 5 Mc, tumekubali.
Brass Band kutoka makutupora JKT ilikuwepo. Inanikumbusha zile enzi za ....Wee kurta!
Kikundi cha Utamaduni cha wasukuma wa Bujora na ngoma ya nyoka. Du inataka moyo!
Bila huyu ....Msukuma hajaanua ngoma; wejemeni!

0 comments: