MAZISHI ya Simba wa vita Mzee Rashid Mfaume Kawawa yanatarajiwa kufanyika leo kuanzia majira ya saa 7 adhuhurihuko nyumbani kwake Madale Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Marehemu Kawawa alifariki jana, majira ya saa 3:20 za asubuhi, katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako juzi alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia afya yake.Akiongea na waandishi wa habari kwa huzuni Ikulu, Raisi Kikwete alisema Mzee Kawawa alifika hospitalini hapo juzi kwa ajili ya kwenda kupima malaria kwa kuwa alikuwa na safari na alienda hapo ili aweze kujitambua kama angekuwa na malaria ajitibie kabla ya kwenda safari yake hiyo.Alisema alipofika hospitalini hapo alipima malaria na kukutwa kuwa hakuwa nayo, na alianza safari ya kurudi nyumbani kwake, kabla hajafika nyumbani kwake hali ilibadilika na waliongozana nae walimrudisha hospitalini hapo na jopo la madaktari walianza kumpima kutambua alikuwa akisumbuliwa na nini. Katika vipimo vya haraka haraka madaktari hao waligundua kuwa sukari yake ilikuwa imeshuka sana na kufikia 0.6 hali ambayo iliwafanya madaktari wafanye jitihada kubwa kumshughulikia kurudisha hali yake ikae sawa. Mbali na kumshughulikia sukari, pia waliweza kugundua kuwa vigo zote mbili zilikuwa hazifanyi kazi na pamoja na jitihada zote mwenyezi mungu alichukua uamuzi wa kumchukua majira hayo. Mwili wa Mzee kawawa unaingizwa Karimjee ktika ukumbi wa karimjee Viongozi wakuu wa kitaifa walikuwepo Karimjee Hall.Mapema Raisi jakaya kikwete alisema kuwa taifa limempoteza kiongozi shupavu aliyepigania uhuru wa Tanganyika na alikuwa ni kiongozi mshauri wa karibu wa taifa enzi za uhai wake.Marehemu aliweza kushika nyadhifa nyingi enzi za uhai wake kama vile Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na vyeo vingine kadhaa.Marehemu Kawawa alizaliwa mkoani Ruvuma Wilaya na Namtumbo, Februari 27, mwaka 1926. Alifariki jana akiwa na umri wa miaka 83.(Picha na M.Michuzi na Full Shangwe)
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment