Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, January 06, 2010

Raisi wa Afrika kusini Jacob Zuma akiwasili katika eneo lililofanyika sherehe ya harusi ya kijadi ili kumuoa Bi. Tobeka Madiba kama mke wake wa tano katika kijiji cha Nkandla kaskazini ya kwazulu Natal na hiyo ilikuwa juzi J3, January 4, 2010. Zuma mwenye miaka 68 amemuoa mwenye miaka 37 kutokana na mila za Wazulu.Tobeka alikuwa naye kwa kipindi kirefu lakini sasa amehalalisha ndoa yake kimila. Hii ni ndoa ya tano . Japo kwa sasa ana wake watatu. Mke mmoja aliwahi kumtaliki siku za nyuma na mke mwingine alikufa. Wageni 2000 walihudhuria japo waandishi wa habari walikataliwa. Unasemaje…Inapendeza au!…Jambo linalowavutia watu ni jinsi Rais Zuma anavyochangamkia hobi yake ya kucheza kwa umahiri Mkubwa . Unaweza kuangalia video hiyo hapo chini kabla ya kuwaona kwa karibu wake zake watatu. Katikati ya burudani... Katikati ya sherehe ya harusi akiwa na Bi harusi...
Wake watatu wa Mh.Zuma.Wa mwisho kushoto ndiye aliyeolewa juziwakiwa na mume wao..

0 comments: