Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, February 01, 2010


DAKTARI wa Hospitali ya Marie Stoppers iliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, Paul Andrew ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyefika hospitalini hapo kupatiwa matibabu.Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga zimesema kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa tumbo ndipo Dk. Andrew alimwandikia kipimo cha Utra Sound.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda Kalinga alisema kwa mujibu wa mgonjwa huyo, alifika hospitalini hapo majira ya jioni na baada ya kueleza tatizo lake, Dk Andrew alimwandikia kipimo hicho.Kamanda Kalinga alieeleza kuwa baada ya kuingia katika chumba cha kufanyiwa kipimo, ndipo daktari huyo alimpa kitu kilichomfanya alale kwa muda na nguvu ya dawa ilipokwisha alishtuka na kumkuta daktari huyo akiendelea kumbaka.“Baada ya kumkuta daktari akimbaka, mgonjwa huyo alitoka na kukimbilia Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na kufungua jalada lenye namba RB/KJN/123/552/10,” alieleza.Alisema askari hao walirudi na mgonjwa huyo hospitali na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa bado yupo eneo hilo.Kamanda alisema mgonjwa huyo amefanyiwa vipimo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kubaini kama kweli alifanyiwa unyama huo.Alisema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi na leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo.habari na Betty Kangonga wa gazeti la Tanzania Daima.
(Kama ni kweli imefanyika hivyo)!!!!Huu ni aina ya ugaidi, sijui unasemaje mdau!

0 comments: