Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, March 06, 2010


Mahakama ya jiji la Nagoya hapa Japani imempiga faini dereva wa lori na kampuni yake ya usafirishaji Yeni 2.9 Millioni sawa na takriban Shillingi za kitanzania Millioni 42 kwa kumgonga kwa gari lake mbwa ambaye aliyekuwa akitumika kuongozea watu barabarani hasa kwa watu wasioona.Shirika linalommiliki mbwa huyo ya Chubu Modekan Kyokai ilifungua kesi mahakamani dhidi ya dereva huyo na kampuni yake akidai alipwe Yeni Millioni 6 sawa na fedha za Kitanzania Millioni 87 kwa kifo hicho cha mbwa akidai ametumia gharama kubwa kumfundisha hadi kufikia hapo.
Jaji Atsuko Matsuda alisema kuwa "Mbwa kiongozi wana thamani kubwa na kwamba gharama za kumfundisha hazina budi kuzingatiwa." Japani wakali , hebu fikiria ingelikuwa binaadamu ingekuwaje hapo.

0 comments: