Mjukuu wa Mfalme wa JAPANI Mwana wa mwana wa Mfalme Princess Aiko ameshindwa kwenda shule kutokana na kile kilchosemwa kuwa ni kusumbuliwa na wavulana.
Binti huyo pekee wa mwana wa Mfalme Crown Prince Naruhito na Mkewe Princess Masako, amekuwa hafurahii kwenda shule tangu Jumatatu wiki hii baada ya "kusumbuliwa" na wavulana wa darasa lake na taarifa hizo kutolewa na Wahudumu rasmi wa makazi ya mfalme.Binti huyo mwenye miaka 8 inasemekana amekuwa akichokozwa na wanafunzi wenzake.Inaelezwa kuwa anasoma katika shule ya msingi Gakushuin eneo la Shinjuku na siku ya kwanza baada ya kupata mkasa huo alionekana kutahayari na kulalamikia maumivu ya kichwa , jambo alilolizungumzia Mhudumu mkuu wa Kasri ya kifalme katika Mkutano wa kawaida na waandishi wa habari.
Mwana wa mfalme Prince Naruhito na mkewe Princess Masako wazazi wa Princess Aiko.
Princess Aiko alikuwa haonekani shule tangu mwishoni mwa mwezi Februari akisumbuliwa na homa na jumanne aliondoka mapema shuleni na hajaonekana tena. Tayari Uongozi wa shule umepewa maagizo kushughulikia suala hilo.Katika Mkutano mwingine na waandishi wa habari Mkurugenzi wa shule hiyo ya msingi Gakushuin Motomasa Higashisono amesema kuwa hana taarifa juu ya kuwepo kwa usumbufu huo.Usumbufu unaotajwa ni pamoja na kupiga kelele kwa watoto, kuusha mabegi, kukimbia kwa kishindo kwenye makorido jambo ambalo Princess Aiko halipendi.
Shule hiyo imekuwa ikitumika na wanafamilia wa kifalme kujiendeleza kimasomo ikiwa ni pamoja na Mfalme mwenyewe Akihito na mkewe Naruhito kama wanavyoonekana katika picha hapo chini..
Suala hilo si dogo limemfikia Waziri Mkuu wa Japani naye amekaririwa akisema kuwa "Aiko kama raia wa kawaida wa Japani ,ninatumaini atapata nafuu na kurudi katika hali yake mapema iwezekanavyo".Nchini Japani Mfalme ni alama ta nchi. Hakuna jambo dogo katika familia ya kifalme. (Habari ; Mainichi Japan)
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, March 06, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment