Tumepokea mtu muhimu katika Ulimwengu wa Muziki , Fresh Jumbe Mwinyi katika studio zetu za NHK hapa TOKYO leo. Tuklikuwa na mazungumzo na baadaye mahojiano studio kwa ajili ya vipindi vya moja kwa moja na mtandao wa intaneti.Mwanamuziki huyu ana historia na hazina kubwa ya habari za muziki katika eneo letu la Afrika Mashariki hususan Tanzania. Kwa vijana wa zamani watakumbuka Enzi ya Dar International, Msondo , Sikinde, OSS , Bicco Stars ambako aliziimbia bendi hizo na kuacha tunzi zake.Mahojiano yetu pia yataanza kusikika kwa mfululizo kuanzia siku ya Alhamisi kwa wasilikilizaji wa Afrika Mashariki na kati na kwa njia ya mtandao pia wa; www.nhk.or.jp/swahili . Unaweza pia kumtembelea katika mtandao wake binafsi kupata habari za karibuni kwa kubofya neno Fresh Jumbe hapo kulia kwako kwenye orodha ya mitandao rafiki ama bofya; www.freshjumbe.com
Ndani ya studio za NHK jijini Tokyo leo Jumatatu kabla ya mahojiano....
Kiongozi mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani Yuko Asano (Kushoto), Mwanamuziki Fresh Jumbe (kati) na nami Kulia mara tu baada ya mazungumzo yetu studioni.
Bi. Yuko asano, Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili Redio Japani aliyejiunga wiki hii kutokea KBC Kenya Mr. Kadilo na Fresh Jumbe Mwinyi (Kulia)
Nje ya studio tukakumbana na flash...Pwaaa!
Nukta chache kabla Fresh hajaondoka B/H.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Monday, April 19, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment