Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.1 kwenye kipimo cha Richter limetokea hivi majuzi huko Yushu katika jimbo la Tibeti mkoani Qinghai, China. inasemekana takriban watu 800 wamefariki na maelfu wamejeruhiwa.
Sehemu zilizokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi ziko kwenye mashariki ya Uwanda wa juu wa Qinghai na Tibet wenye mwinuko wa zaidi ya mita 4400 kwenye usawa wa bahari, hivyo kazi ya kuwatafuta na kuwaokoa watu waliofunikwa chini ya vifusi inakabiliwa na taabu nyingi kubwa.Fuatilia hali ilivyokuwa na ilivyo sasa kwa njia ya picha.
Makasisi wa dini za kijadi wakiwa mbele ya jengo la bweni lao katika mji wa Jieng, eneo la Yushu , Qinghai huko China.
Hali halisi ndio hii...
Picha iliyopigwa muda mfupi baada ya tetemeko hilo.
Maafa makubwa.
Utafutaji wa manusura ; kazi inapokuwa ngumu.
shughuli za uokozi zinaendelea kufanywa na vikosi mbalimbali kikiwemo hiki cha wanajeshi.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, April 17, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment