Bibi mwenye umri wa miaka 72 wa nchini Marekani amewashangaza marafiki zake na familia yake baada ya kutoboa siri kuwa anatarajia kuzaa mtoto na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 26.Bibi Pearl Carter, 72, anasema kuwa hajawahi kuwa mwenye furaha kama wakati ambao amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wake Phil Bailey mwenye umri wa miaka 26.Bibi huyo wa Indiana, Marekani anatumia pesa zake za pensheni kumlipa mwanamke atakayejitolea kuibeba mimba yake na mjukuu wake.
Bibi Pearl alisema kuwa hajali maneno ya watu kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi na mjukuu wake na anasubiria kwa hamu kuzaa naye mtoto.
Phil ni mjukuu wa bibi Pearl kwa mtoto wake wa kike Lynette Bailey ambaye alipelekwa kwenye nyumba ya kulea yatima alipokuwa na umri wa miaka 18.Wakati mama yake alipofariki, Phil alimtafuta bibi yake ambaye alikuwa hana mawasiliano naye kwa muda mrefu na ghafla walianza uhusiano wa kimapenzi."Ilikuwa ni wiki ya pili pamoja baada ya chakula na mvinyo nilipomuita Phil chumbani kwangu, nilimkalisha kitandani na kuanza kumbusu", alisema bibi Pearl."Nilitarajia angenikatalia lakini naye alianza kunibusu" Pearl alisema akielezea mwanzo wa uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wake.
"Kwa mara ya kwanza nilijihisi kwenye msisimuko mkubwa wa kimapenzi", alisema bibi Pearl.Phil naye kwa upande wake anasema kuwa anampenda sana bibi yake na kwakuwa tangia zamani alikuwa akiwapenda wanawake wazee anadhani bibi yake ni mrembo sana.
Phil na bibi yake wametumia dola 54,000 kumlipa mwanamke atakayebeba ujauzito wao.
"Ni kweli tunachekwa na kutukwana wakati tunapobusiana mbele za watu lakini hatujali kitu", alisema Phil."Sitamuomba radhi mtu yoyote kwani naamini Mungu amenipa nafasi ya pili", alimalizia kusema bibi Pearl.
Maagizo ya rais ni nini?
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment