Mkurugenzi wa bendi ya Bwagamoyo Sound Internationale Prince Muumin Mwinjuma akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akielezea maendeleo ya bendi yake iliyokuwa imepiga kambi mkoani Tanga huko Chumbageni.
Prince Muumin Mwinjuma amesema tayari bendi yake imeshajiimarisha na inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 4 Juni mwaka huu kwenye ukumbi wa Vatcan City Sinza jijini Dar es salaam ili kuonyesha kazi yao iliyowafanya kuwepo kambini Tanga kwa muda mrefu.
Ameongeza kwamba katika uzinduzi huo kutakuwa na bendi ya Taarab ya Jahazi Molden Taarab inayoongozwa na Mwanamuziki mashuhuri nchini katika muziki wa taarab Mzee Yusuf, pia kutakuwa na bendi kongwe nchini ya Msondo Music Band na burudani nyingine lukuki.
Amesema kuwa katika onesho hilo pia wanatarajia kumtambulisha mwanamuziki wao mpya Kalama Legesu (Pichani Kushoto)ambaye wamemchukua kutoka bendi ya Mlipani Park Orchestre (Sikinde)ya jijini Dar es salaam ili kuimarisha kikosi chao na akaongeza kwamba kabla ya kuondoka mkoani Tanga watafanya onesho moja la kuwaaga wakazi wa mkoa wa Tanga.Amemalizia kuwa Albam yao mpya katika bendi hiyo ina nyimbo 6 na imepewa jina la “Nafsi haina Urithi”
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, May 09, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment