Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, June 03, 2010

SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa zaidi ya shilingi bilioni 74 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya Bagamoyo kupitia Mwenge


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, alisema msaada huo wa fedha utasaidia kupunguza foleni katika barabara hiyo pindi ujenzi huo utakapokamilika.Alisema barabara hiyo, ina urefu wa kilomita 12.9 italeta maendeleo na kurahisisha suala zima la usafiri na kuondoa kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari unaosababisha kuwepo kwa foleni.Pia alisema upanuzi huo utalazimu nyumba zilizopo kando ya barabara hiyo kubomolewa kwa kuwa mafundi wataingia ndani mita mbili kila upande wa barabara hiyo kuanzia Mwenge, Tegeta hadi Bagamoyo ili kupisha ujenzi huo.Alisema wakazi wote watakaobomolewa nyumba zao, watalipwa fidia kutokana na tathmini itakayofanyika kila mtu atapewa fidia yake kwa kigezo cha uthamani wa nyumba itakayobomolewa. *Picha na Sufiani Mafoto...(Take 5 Bro.)

0 comments: