Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, June 03, 2010


Mwanamke mmoja nchini Iran amemfikisha mumewe mahakamani akidai talaka kwakuwa mume wake hajawahi kumpiga hata siku moja.Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 alifungua kesi katika mahakama ya masuala ya familia mjini Tehran akilalamika kuwa mumewe hampigi hivyo anataka apewe talaka.
Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku la nchini Iran, mwanamke huyo aliiambia mahakama "Mume wangu ananitumikia na kunitunza vizuri sana lakini mimi nataka awe ananipiga, kama hawezi basi naomba anipe talaka yangu".Mume wake ambaye ana umri wa miaka 28 alijitetea mahakamani "Mke wangu nampenda sana, sioni sababu ya kumpiga au kutumia maguvu dhidi yake".Kwakuwa mwanamke huyo alisisitiza kuwa anataka awe anapigwa na mumewe au la apewe talaka, mahakama ilimruhusu mumewe awe anamshushia kipigo mkewe siku moja moja ili kuilinda ndoa yake, umekaririri mtandao wa www.nifahamishe.com .Mumewe kwa shingo upande alikubali na aliahidi kuwa atakuwa akimshushia kipigo mkewe ili kumridhisha.

Ushauri wa bure kama anataka kipigo cha kuua nyoka akaolewe na watani zangu Waku...kule nyumbani.

3 comments:

Anonymous said...

Mkuu salamu. Pole kwa kuugua mafua. Ila ujue tuu kuwa JAPANI hakuna kipindi(season) yeyote ambao ni safe free from FLUE/ coughing etc!

Mkuu hii page ya leo kuhusu mamy anaetaka kupigwa for love imenifurahisha sana. Ninaommba if possible unipe link niweze kuisoma kwa kiingereza ili niweze kushare na dnuguzangu pia.

Asante
Pajoma

Anonymous said...

Pole na majukumu Pajoma, nimefurahi kwa kuitembelea Mirindimo. Unaweza kutembelea mtandao wa ; www.nifahamishe.com kwenye column ya life style unaweza kukumbana na taarifa nyingi za kuduwaza. Mbali na hili nitafurahi kupokea picha na taarifa za kusisismua kutoka kwako ambazo tunaweza kuziweka kwenye Mirindimo. Nakutakia afya njema.
bm.

Anonymous said...

Mheshimiwa ni kweli nilibanwa na mafua na yalitingisha . Kwasasa nimeanza kurejea kati hali ya kawaida na matumaini kuwa wiki moja ijayo nitakuwa fit zaidi.Shukran sana.