Kumbuka; taarifa hii imenakiliwa neno kwa neno kutoka blogi ya nifahamishe-BM.
Msanii mkongwe hapa chini wa muziki wa Bongo Fleva, Mr II aka Sugu anatamba na albamu yake Anti Virus ambayo ndani yake kuna nyimbo ambayo ametaja watangazaji wa radio Clouds anaodai wanasambaza ukimwi huku wengine akiwataja kuwa ni mashoga.
Msanii mkongwe hapa nchini Joseph Mbilinyi aka Mr 11 Sugu, ameliteka jiji la Dar kutokana na albamu yake ya Anti Virus ambayo ndani yake amewapaka live watangazaji na viongozi wa redio ya Clouds FM.KWa mujibu wa Mr II watangazaji hao wanadaiwa kutumia redio hiyo kwa kuwatongoza wanawake wanaokwenda pale kuomba kazi pia kuzibania kazi za wasanii ambao hawapo katika listi yao.Mr II pia amewachana live kundi la THT Kituo cha kukuza vipaji Tanzania Kuwa kituo hicho kinatumika kinyume na ilivyotarajiwa.Albamu hiyo ya Sugu ina nyimbo zaidi ya 14 lakini hapa nchini haziwezi kupigwa katika vituo vya redio kutokana na kujaa matusi ya hadharani, hivyo albamu hiyo imekuwa ikiuzwa chini kwa chini na watanzania wengi wamekuwa wakiishambulia kwa kuinunua hasa wale wapenda mapinduzi katika fani hiyo ya muziki wa kisasa kwani vijana wengi wamekuwa wakibaniwa kazi zao kutokana na kutofahamika au kutokana na kutokuwa na uhusiano muzuri na watu wa redio na Tv.Majuzi Sugu alikamtwa na polisi na kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano, lakini baadaye aliachiwa kwa dhamana.MR II amewaweka njia panda watangazaji wa Clouds hasa kwa kuwataja live baadhi ya watangazaji kuwa wanasambaza Ukimwi kwa makusudi huku wakijua kuwa wao ni waathirika wa ugonjwa huo.Pia aliwataja baadhi watangazaji kuwa ni wasenge jambo ambalo limewafanya watu wengi wajiulize imekuwaje hadi Mr II ameamua kutunga nyimbo hiyo na kuisambaza kwa watanzania?.
Mmmh Mi sichemi!
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Monday, July 05, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment