Maveterani watatu wa vita kutoka nchini Marekani wakiwa na ulemavu wa viungo, kila mmoja akiwa na mguu mmoja ulio mzima na mwingine akiwa na miwili yote ya bandia wamefanikiwa kufika kileleni katika mlima Kilimanjaro, Mlima ulio mrefu kuliko wote barani Afrika.
Neil Duncan, 26, alipoteza miguu yake yote kutokana na bomu lililotegwa kando ya barabara huko Afghanistan mwaka 2005;
Maveterani hao wa vita , walishiriki katika vita nchini Vietnam, Afghanistan na Iraq walifika kilele cha mlima huo takriban mita 5,891 juu ya usawa wa bahari sawa na futi (19,330ft). Walitumia siku sita na kudhihirisha kuwa ulemavu sio kutoweza kila.
Wapandaji hao wa mlima walikuwa Dan Nevins, mwenye miaka 37, aliyepoteza miguu yake yote nchini Iraq;
Neil Duncan, 26, alipoteza miguu kutokana na bomu lililotegwa kando ya barabara huko Afghanistan mwaka 2005; na Kirk Bauer, mwenye umri wa miaka 62, alipoteza mguu mmoja katika vita vya Vietnam mwaka 1969.
Dan Nevins,(37)Duncan,( 26), Kirk Bauer(62)
Walipofika Kwenye kituo cha Gillman wakielekea kileleni walionekana na majeraha madogomadogo katika mapaja lakini wakiwa na furaha tele..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, August 14, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment