Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, September 05, 2010

Shirika la Utabiri wa hali ya hewa ya Japani imesema kuwa , Joto kali linaloendelea nchini Japani hususan Tokyo liliwahi kutokea mwaka 1946 , wakati huo ukusanyaji wa takwimu za hali ya joto ulipoanza baada ya vita vya pili vya dunia.

Visiwa viwili vya Japani ndio hali yake imebakia kwa kiasi fulani na joto lililooeleka vya Amami na Okinawa. Miji yote mikubwa vipimo vya wastani vya joto vinaonyesha kuwa juu , Kyoto ikifikia 30.0, Osaka 30.4 , Hiroshima 30.3 na Fukuoka 30.4 wakati jiji la Tokyo wastani wake ulifikia nyuzi 29.5 hadi 32 wakati mingine. Na kibaya zaidi joto wakati wa usiku katika jiji la Tokyo liliendelea kubaki Nyuzi 25.9 wakati fulani na wataalamu wanasema kuwa hii ilitokea miaka 113 iliyopita, japo kwa sasa limepungua kidogo.

Watu kadhaa hususan wazee wanaelezwa kuwa wamepoteza maisha yao kwa ajili ya joto hili


Watu sasa wanalazimika kuvaa vivazi vyepesi, miamvuli na kujifunga mataulo yenye unyevunyevu kupunguza lawama, na nyakati za jioni kwenye fukwe, bichi , chini ya miti watu hujazana. Na wengineo hukaa majumbani mwao wakipigwa na upepo wa mashine.Balaa...

0 comments: