Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, September 05, 2010

Genge la watu sita likiongozwa na kijana mmoja wa Ki-Nigeria Nyenche Obenene limekamatwa katika jiji la Tokyo likituhumiwa kuhusika na wizi wa fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia mitandao ya kibenki.

Polisi jijini Tokyo wamesema kuwa watu hao wamejipatia takriban Yeni Millioni 570 kutoka benki ya Marekani katika jitihada zinazotajwa za kuziingiza katika mkondo halali wa kifedha. Fedha hizo na matrilioni kadhaa kwa fedha za Tanzania.

Mtuhumiwa Nyeche Obeneme, ana miaka 36 na mmoja wa wakurugenzi waandamizi wa Kampuni moja inayosafirisha magari iliyopo Mkoa wa Saitama hapa Japani , eneo la Okegawa ambaye ameshirikiana na Wa-Nigeria wenzake wawili, mwanamme mwingine wa Ki-Ghana na wajapani wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanaume.
Fedha hizo zinaaminika kuwa ni sehemu ya YENI Billioni 2.8 zilizosambaza kwa njia ya mtandao kwenye mataifa saba zikiwemo Japan, Korea Kusini, China na Australia na hii ni kwa mujibu wa dodoso kutoka kwenye akaunti ya Citibank iliyopo New York ikiwa na jina la National Bank of Ethiopia in the autumn of 2008.
Fedha zilizoletwa Japani Yeni Millioni 570 zimekwishachukuliwa Benki na sasa Polisi wanahaha kujua nani kapitiwa na fedha hizo. Habari zinasema kuwa Wa-Nigeria watatu wamekamatwa huko Korea Kusini walipokuwa wakijaribu kuchukua sehemu ya fedha hizo na Mnigeria Mwingine amekamatwa alipokuwa akijaribu kughushi nyaraka bandia za kusafirishia pesa kwenda kwenye Benki ya Citibank. Polisi wameapa kuwa hata yule aliyekula yeni moja atanaswa tu . ……Kazi kwelikweli!

0 comments: