Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, September 20, 2010

Mkoa wa Kanagawa nchini Japani si sehemu inayofaa kwa mtu anayevuta sigara . Mkoa huo ambao unajumuisha jiji la Yokohama una sheria inayowazuia watu kuvuta sigara hadharani , mitaani na katika majengo ya umma.

Mji Mkuu wa Mkoa wa Kanagawa , Yokohama.

Ikikulazimu kuvuta inabidi uende kwenye vibanda maalum ama kwenye migahawa inayoruhusu kuvuta. Mtu akipatikana na hatia faini yeni Elfu hamsini sawa na Fedha za Ki-Tz Millioni nane na ushee. Maeneo ambayo ni marufuku kabisa ni pamoja na hospitali, shule na kadhalika. Wadau napendekeza sheria hii ianze kutekelezwa katika majiji ya Dar na Mara ..mnasemaje!

0 comments: