Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, September 20, 2010

Japani leo Jumatatu ni siku ya mapumziko kuwaenzi wazee. Nataka tuangalie wastani wa umri wa kuishi hapa Japani na maeneo mengine duniani.

Huyu bibi alikwishavunja rekodi ya kuwa mwanamke mwenye umri mkubwa duniani baada ya kutimiza miaka 114 . Bahati mbaya amefariki hivi karibuni.Jina lake ni Yone Minagawa, na hati mauti alikuwa ana fahamu zake na alikuwa akiongea na waandishi wa habari akiwa na uelewa tu wa historia yake.
Wastani wa miaka ya kuishi kwa wanawake wa kijapani sasa umefikia miaka 87 huku akinababa wamefikia miaka 80 na kwa wanawake ni umri mkubwa kuliko wowote duniani, huku akinababa wakishika nafasi ya tano.


Washauri wa kitiba na saikolojia hawachezi mbali na wazee hawa hapa Japani...ndio maana wameendelea kuwepo...
Ofisi za takwimu hapa Tokyo zinasema kuwa watoto waliozaliwa mwaka jana wanatarajiwa kuishi hadi mwaka 2095 au 2096. Kwa miaka 25 wanawake wa kijapani wamekuwa wakiongoza kuishi maisha marefu duniani wakifuatiwa na wenzao wa Hongkong miaka 86.1, Ufaransa 84.5, Uswisi 84.4 na Uhispania miaka 82.27.
Kwetu Afrika
nchi yenye wastani mdogo kabisa wa kuishi watu wake na inaongoza pia duniani kwa hali hiyo ni Swaziland 33.2 wakifuatiwa na Botswana miaka 33.9 Lesotho wao wastani ni miaka 34.5 Ukivuka umekopa..

Waswaziland katika ngoma ya asili...
Tanzania wastani wa kuishi wanaume ni miaka 55 na wanawake 56. Mtu akivuka hapo atakuwa amekwepa mishale mingi ya maisha au siyo!

Boma la kimasai kule kwetu 55 kwa 56 ...du!

0 comments: