Vyakula vya kijapani vina ladha nzuri na za kipekee. Napenda leo nikuelezee staftahi au kifungua kinywa cha kiasili cha wajapani. Kwa mjapani halisi kabla hajatoka kwenda kwenye kazi zake, lazima apate mlo wa asubuhi uliotimia. Menyu hiyo huwa na vitu vifuatavyo;
1.Bakuli la wali lililo na ujazo wa wastani
2.Mnofu wa samaki wenye rangi nyekundu , samaki anayeitwa salmoni ambaye kwa kawaida ana chumvi kidogo na baadhi ya wajapani wanaondoa ngozi yake wakidai hawaipendi.
3.Achali yenye mchanganyiko wa matango, figili na bilinganyi. Huwa nhaivurugwi inakuwa vipande vidogoX2 , zinachovya tu kwenye maji ya moto.
4.Matunda yanayofanana na zambarau yakiwa katika hali ya uchachu..
5.Bakuli la supu ya miso . Supu ya miso hutengenezwa kwa njia mbalimbali lakini ile miye ninayoijua ni mchanganyiko wa mboga za majani na nyama inayowekwa kwenye mchuzi wa uyoga, karoti, viazi mviringo na samaki.
Miso
Viambato hivi huwa katika hali ya vumbi, huchanganywa katika maji. Mabamia yanaweza kuonekana yakielea juu ya supu hiyo na kuleta hali Fulani ya kupendeza. Kwa wageni wanaweza wasiielewe…inakuwa kama miti shamba hivi lakini wenyewe wana-injoiii!
6.Bakuli la maharagwe ya soya yaliyochachushwa
7.Na Kibakuli cha mwani (Maarufu kule Zanzibar) unavuliwa baharini . Huwa unawekwa na kuelea kwenye kibakuli chenye maji moto
Mlo umetimia….Maswalii!
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, September 28, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Tamu sana hii. Chakula chenye afya kabisa mwilini. Nawapenda sana hao samaki wakiwa wabichi utie limao kidooooogo na chumvi kidoooogo au bila, mwe, utajing'ata kidole walahi.
Sasa nimepata picha ni kwanini hawa jamaa wanaishi miaka mingi zaidi kuliko binadamu wengine duniani.
Jamaa hawabahatishi...wanakula vya kutosha , wanafanyakazi vya kutosha na wanafuatilia afya zao. Na kubwa wanachoambiwa na daktari wanakifuata kama amri kuu. Hawa jamaa bwana Mmh!
Chembelecho wahenga ,Uhai unaanzia kwenye mlo.
Post a Comment