Lengo na madhumuni makubwa ya kufika hapa Yokohama ni kuhudhuria maonyesho ya sanaa ya tingatinga. Aina maalum ya michoro ambayo asili yake ni Tanzania. Kwanza pitisha macho halafu nikutambulishe kwa mchoraji..Mustapha Abdallah...
Jamaa akiwa mzigoni ..huyu jamaa abnnaitangaza Tanzania saana tu kupitia tingatinga.
Pozi na Mustapha..
Mh. huyu anaitwa Shizuoka na sasa anajina jipya anaitwa Abdul Halim baada ya kusilimu. Amekaa Zanzibar kwa miaka 25 akiwa na mkewe Yumiko. Wanaongea Kiswahili vizuri. Anasema ameanzisha kampeni ya kuitangaza Afrika na hasa Tanzania vizuri duniani. Kwa maneno yake wajapani wengi hawaijui Tanzania na bidhaa zake nzuri kama vile kahawa, chai na tingatinga. Huyu Bwana na mkewe ndio waliomleta Mustapha hapa japani ili kuitangaza tingatinga. Tumefanya mahojiano naye na ikifika siku ya siku nitawajulisha jinsi ya kuyasikiliza mahojiano hayo.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, September 03, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment