Mama mmoja nchini Japani jana inasemekana alimuua mtoto wake wa kike mwenye miaka mitatu kwa kumchoma kwa kisu.Tukio hilo lilianzia pale mtoto wa kiume wa mama huyo mwenye miaka tisa alipopiga simu polisi kuomba msaada na ndipo Polisi walipofika na kumkamata mama huyo mwenye umri wa miaka 41.
Miundombinu eneo la Konohana -Osaka..
Mama huyo alikutwa amejilaza kwenye dimbwi la damu akiwa na mtoto wake huyo aliyemchoma kisu aliyekuwa akipumua kwa taabu katika nyumba yao eneo la Konohana katika jiji la Osaka. Jitihada za polisi kuokoa maisha ya binti huyo mdogo zilishindikana. Mtoto wa kiume aliyepiga simu Polisi alikutwa na jeraha dogo mkononi inaelekea alikuwa akisaidia kumuokoa mdogo wake.
Polisi wamesema kuwa huenda mama huyo alikuwa katika jaribio la kujiua baada kufanya kitendo hicho lakini baada ya kupata maumivu yakamshinda...Mbali na mtoto huyo aliyemuua wa miaka mitatu na yule wa kiume wa miaka tisa pia ana mtoto wa kike wa miaka 12.Mtoto huyo wa kiume aliwaambia Polisi kuwa mama yao alianza kuonyesha tabia zisizo za kawaida tangu mapema asubuhi jana Jumamosi. Mama huyo aliachika miaka kadhaa iliyopita na amekuwa akiishi na wanawe hao watatu.Polisi wanaendelea na uchunguzi...
Maagizo ya rais ni nini?
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment