Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, November 21, 2010

Asubuhi ya saa mbili na robo August 6, mwaka 1945 ilikuwa siku mbaya sana kwa wajapani pale majeshi ya Marekani yalipoamua kudondosha bomu la maangamizi katika miji ya HIROSHIMA na NAGASAKI hapa Japani. Hii ikiwa ni mara ya kwanza na haijafanyika tena katika dunia hii. Bomu hilo limedondoshwa mita 600 tu kutoka kitovu cha Jiji la Hiroshima ambalo wakati huo uchumi wake ulikuwa ukikua kwa kasi...Fuatilia picha chache za kuanzia juu ya tukio hilo...

Safari na mgeni wetu Bw. Franz Ngogo ya kwenda Hiroshima iliendelea tena . Tulitumia usafiri wa treni ziendazo kasi zinazojulikana hapa japani kama Shinkasen(Pichani) Kilometa 300 kwa saa ...



Safari imeanza ....

'V' Alama ya 'Amani' kwa Wajapani, tulikutana na wanafunzi hawa waliokuja kutembelea eneo hili.


Inaelezwa kuwa watu takriban 140,000 walikufa kutokana na bomu hilo lililodondoshwa na Majeshi ya Marekani mwishoni mwa vita ya pili ya dunia.



Mabaki yanayohifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu ya kizazi kijacho....
Mbele kabisa mwa Jengo lililoteketezwa na bomu hilo ...

Bomu hilo lilikuwa na uzito wa tani nne liliangamiza eneo hilo kwa sekunde chache tu, na inaonyesha kuwa joto lililotokana na kuangushwa kwake lilifikia sentigredi elfu tano. Hebu fikiria ...kila kitu kiligeuka vumbi...Watu waliokuwa umbali wa Kilometa mbili kutoka hapo walipata madhara makubwa na ni wachache tu waliendelea kuishi na kufa baadaye...wachace mno wapo hivi sasa lakini wanaulemavu wa kudumu...

1 comments:

Simon Kitururu said...

Binadamu wanasahau kirahisi sana afadhali kumbukumbu kama hivi zinahifadhiwa.

Ila chakujiuliza:
Hivi kweli binadamu wamejifunza kitu ukizingatia ndio kwanza nia za kutengeneza mabomu ya aina hiyo yaliyoleta madhara hapo ndio ndio kwanza inakua na kuenea kwenye nchi mpya nyingine?