"Tusambaze mbegu ya amani kote duniani , nuru ya jua inamaanisha nini kwangu?"
Huu ndio ujumbe na mada ya mwaka huu ya mashindano ya insha ya Kiswahili yanayofanyika kila mwaka katika chuo Kikuu cha Soka nchini Japani ambapo wadau mbalimbali raia wa Japani hushiriki kuandika na kuwasilisha mada zao mbele ya Majaji.
Safari hii mchuano ulikuwa mkali:
Mwanafunzi wa soka Unversity Ruri Ookubo aliyeshika nafasi ya tatu ...
Kati ya washiriki nane , wanawake sita na wanaume wawili Bi Haluka Nakamula (Aliyevaa bazee hapo chini)ambaye naye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu ca Soka alipata pointi kadhaa ambazo zilimuwezesha kushika nafasi ya pili baada ya kujibu kwa ufasaha swali la mmoja wa majaji wa shindano hilo.
Mshindi wa kwanza wa shindano hilo Bi Tomoni Kosugi Grellan akipokea kikombe cha ushindi baada ya kujinyakulia ushindi huo. Balozi wa Tanzania hapa Japani Mh. Salome Sijaona ndiye aliyemkabidhi zawadi hiyo. Katika hotuba yake alikisifu sana kiswahili kwa kusaidia kulifanya eneo la Afrika Mashariki kuwa na mawasiliano, na pia uwepo wa ushirikiano na amani nchini Tanzania ambako kuna makabila zaidi ya 120. Na kukubaliana na dhana kuwa Kiswahili ni lugha ya amani.
Mmoja wa majaji wa shindano hilo Anna kwambaza wa Redio Japani akiteta na baadhi ya washiriki baada ya shindano hilo kumalizika. Nilimuuliza kama kulikuwa na 'uchakachuaji' wakati wa mchakato huo , akatabasamu tu. NO ilikuwa fair. Majaji wengine walitoka katika balozi za Kongo DRC na Kenya.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, November 05, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment