Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, November 30, 2010

Polisi wa Yokohama katika mkoa wa Kanagawa wametoa taarifa rasmi kuhusiana na taarifa za kukamatwa kwa watanzania na madawa ya kulevya . Wamesema kuwa wamewakamata watanzania wawili baada ya kuthibitika kuwa walimeza dawa za kulevya aina ya Heroin katika matumbo yao.Wakwanza aliyetajwa kuanguka kwenye mikono ya wajapani ni Machenga Machenga Ally mwenye umri wa miaka 33 na Ally Mohamed Husein (37) ambao wanadaiwa kumeza kilogram 1.3 za heroin zenye thamani ya fedha za Japani zipatazo Millioni 78 kulingana na Polisi wa mkoa wa Kanagawa. Yeni Millioni 78 ukitaka kujua kwa fedha ya Tanzania zidisha (78,000,000 x 17.1)'hesabu zangu'.


Polisi hao wa Mkoa wa Kanagawa walisema kuwa Watanzania hao walikamatwa jumanne iliyopita ya Nov.23 wakiwa na kapsuli 5 kila mmoja zikiwa na gramu 13 za heroin zikiwa nyuma ya gari walilokuwemo. Awali Machenga Ally alimeza Kapsuli( capsules) 25 zenye ukubwa unaofanana na huo na tarehe 24 siku ya jumatano walilazwa hospitalini ambapo Machenga Ally alivitoa kwa njia ya haja kubwa kapsuli 10 na Husein kapsuli 40 Polisi wamesema kuwa watuhumiwa hao ambao wamekiri makosa yao waliondoka Tanzania tarehe 19 Novemba siku ya Ijumaa na kuingia Japani Novemba 22. Kilichowaponza kulingana na maelezo ya Polisi ni kuwa wenyeji wao katika eneo walilofikia alitoa taarifa Polisi katika mkoa huo wa Kanagawa kuwa jamaa zake walikuwa wakilalamika kuwa wanaumwa sana tumbo jambo liliwatia mashaka, hatimaye kila kitu kikawa hadharani.

Hata hivyo kuhusika ama kutohusika kwao kutafahamika pale watakapofikishwa mahakamani na ukweli ukabainika. Kwa sasa wanabakia kuwa watuhumiwa...Magazeti mengi ya Japani hii leo yamekuwa yakitoa fursa watu kutoa maoni yao na mmoja alikuwa akiulizia Tanzania iko wapi....huyu vipi!

0 comments: