Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, December 29, 2010

Polisi nchini Japani wamepeleka ripoti yao kwa waendesha mashitaka kuhusiana na Maafisa wa uhamiaji 10 wanaotuhumiwa kumshambulia raia mmoja kutoka nchini Ghana , wakidai kuwa mghana huyo aliyekuwa akisafirishwa kwenda kwao mwezi Machi aliteswa jambo lililosababisha kifo chake.


Vyanzo vya uchunguzi huo vilibainishwa jana Jumanne na kuchapishwa katika mitandao kadhaa hapa Japani. Ingawa hawajakamatwa , maafisa hao wanatuhumiwa kuhusika na kifo cha Abubakar Awudu Suraj mwenye umri wa miaka 45 aliyekufa baada ya maafisa kadhaa kutumia nguvu alipoonekana kuleta ‘Upinzani’ wakati wa kumuingiza ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa Narita. Ndege hiyo ilikuwa ikielekea ikielekea Cairo nchini Misri. Mgahana huyo anadaiwa kuwa alikuwa akiishi nchini Japani kinyume cha sheria na hivyo ilikuwa harakati za maafisa hao za kumrudisha kwao na hii ilikuwa mwezi machi, vyanzo vya habari vilibaini.

Polisi huko Chiba nje ya Jiji la Tokyo walisema mapema kuwa uchunguzi wa mwili wake katika Postmortem ulibaini kuwa hakukuwa na majeraha nje ya mwili wake , wala kuvunjwa kwa mifupa, ugonjwa na sababu nyingine zinazoweza kusababisha kifo hicho lakini mwezi Juni Mjane wa Suraj mwenye umri wa miaka 49 alifungua shauri hilo pamoja na waendesha mashitaka dhidi ya maafisa hao wa uhamiaji. Tuhuma kulingana na shauri hilo linawashutum maafisa wa uhamiaji kumjeruhi na kusababisha kifo chake wakati wakati wakimsafirisha kwenda kwao.


Ofisi moja katika kitengo cha uhamiaji cha jiji la Tokyo ambayo maafisa hao wanaotuhumiwa wanafanyia kazi jana jumanne walieleza utayari wao wa kushirikiana katika uchunguzi wa suala hilo.

Tamko hilolinasema kuwa “Tutaendelea kushirikiana katika uchunguzi na kwamba watatoa ushirikiano unaohitajika kwa watu wote wanaohusika na suala hilo ikiwa ni pamoja na familia yake kuhusiana na ucunguzi wa suala hilo.

0 comments: