Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, December 28, 2010

Supu bia , thupu thoda ….kumbe supu ya mbwa! Watu bwana .Wakazi wa mjini Tabora, wamejikuta wakila mbwa bila kutaka baada ya baadhi ya bar kuaanza kutumia mbwa kwa supu na nyama choma.


Maafisa afya waandamizi katika halmashauri ya manispaa ya Tabora, ambao hata hivyo wameoomba majina yao yahifadhiwe juzi walikuta mbwa akiwa amekatwakatwa viungo, kutolewa utumbo na kuhifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi kwa ajili ya kupelekwa bar.
Maafisa hao walikuta mkasa huo jirani na bar moja maarufu kwa nyama choma na supu ambapo maafisa hao walituma watu vibarua kufanya usafi katika eneo hilo lililokuwa na nyasi nyingi.
Hata hivyo wahudumu hao waliokuwa wakifyeka, walikuta mfuko huo wa sandarusi ukiwa na nyama ndani ambayo hata hivyo ilikuwa bado inavuja damu kitu ambacho kiliwafanya wawe na hofu huenda ikawa ni mtoto amecharangwa mapanga na kutupwa.
Wahudumu hao waliamua kuwasiliana na maafisa hao wa afya, ambao walifika na kujionea hali halisi ambapo nao walipata fikra kama hizo, hivyo kulazimika kupiga simu polisi kwa ajili ya ufumbuzi zaidi.

Polisi walipofika eneo la tukio, walikuta hali kama hiyo na walipoamua kutoa kitu hicho katika mfuko, awali walidhani kuwa ni nyama ya mbuzi, baada ya kuona nyama iliyochunwa vizuri na kukatwa kwenye magoti.
Lakini ilipotoka ngozi kichwa na miguu mambo yakawa tofauti, hali ya kutayahari ikaiibuka na ukweli kuhusu supu na nyama choma ukabainika. Askari mmoja alisema kumbe tumekuwa tukilishwa nyama za mbwa jamani watu hawana huruma.
Huku afisa afya akilalamika kwa sauti kuu Lahaula. Jamani dunia sasa imefikia hatua mbaya watu wanatulisha nyama za mbwa kulikoni. Hata hivyo nyama hiyo ya mbwa haikuweza kufika sokoni kwani iliharibiwa kwa mafuta ya taa na kufukiwa.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi (Dullonet)umebaini kuwa mbwa waliokuwa wakizurula hovyo mitaani (Maarufu kama Mbwa koko)katika mji wa Tabora, sasa wametoweka na pengine sababu kuu ya kupungua kwao ni kugeuzwa kitoweo katika bar maarufu na zile za mitaani.
Hii ni habari mbaya kwa wakazi wa Tabora, ambao sasa watalazimika kuchunguza kwanza kabla ya kuvamia supu na nyama choma mitaani katika kipindi hiki cha kuelekea Mwaka mpya. Du! Thanks Dullonet…

0 comments: