Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, January 14, 2011

Mahakama ya hakimu mkazi katika eneo la Utsunomiya hapa Japani leo Alhamisi imemjulisha rasmi mtu aliyeachiliwa huru kutokana na kesi ya mauaji ya mwaka 1990 kuwa atapokea takriban yeni Millioni 80 (takriban (Fedha za kitanzania -1,360 millioni ) kama fidia kutokana na kuhukumiwa kwa makosa .
Mji wa Utsunomiya...

Kiasi hiki ndicho alichodai kulipwa kama fidia.Toshikazu Sugaya, mwenye miaka 64, alidai alipwe fedha hizo mwezi Septemba mwaka jana chini ya sheria ya fidia ya masuala ya kijinai kutokana na msongo mkubwa wa mawazo aliyokabiliana nao katika kipindi cha miaka 17 na nusu alichokaa gerezani.Sugaya alinukuliwa akisema baada ya kupata taarifa hiyo kutoka Mahakamani kuwa “Kiwango hicho ni sawa ‘‘. Mjapani huyo, Sugaya alifungua madai ya fidia baada ya mahakama kumuona kuwa hana hatia pale kesi hiyo iliposikilizwa upya mwezi machi mwaka uliopita akihusishwa na kifo cha binti mdogo wa miaka minne huko Ashikaga, mkoani Tochigi.
Toshikazu Sugaya alikamatwa mwaka 1991 na alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2000 na ndipo alipokata rufaa na kesi yake kusikilizwa upya mwaka 2001 na kuibuka kidedea na millionea. Ingawa awali mahakama hiyo ya ilitupilia mbali ombi hilo mwaka 2008 , Mahakama ya kuu ya Tokyo iliipokea rufaa hiyo kutoka kwa mwanasheria wake akiwakilisha matokeo ya vipimo vipya vya vinasaba -DNA , May, 2009 ambavyo vilithibitisha kuwa hana hatia na wala hakuhusika kabisa na mauaji hayo. Mwezi mmoja baadaye aliachiliwa huru kutoka gerezani.

0 comments: