Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, January 19, 2011

Tulio wengi twapenda kutafuna Chingam, wengine wakiita bazoka , Big G, n.k lakini ikiwa utaitafuna tafadhali sana ujue mambo mbalimbali yanayokukabili kiafya.

1. Utafunaji huo wa Chingam unazeesha tishu ambazo hufanya kazi mithili ya shokomzoba katika viungio vya taya lako. Eneo hili likitumika mno linaathirika na hivyo kukuletea maumivu na kukukosesha raha maisha yako yote.
2. Ufahamu kuwa unatumia misuli nane tofauti ya usoni . Utafunaji usio wa lazima wa chingamu unawezakukuletea hali sugu ya ya kukaza misuli katika misuli ya aina mbili ama tatu kati ya hiyo nane ili karibu na panja (paji la uso) lako. Hali hii husababisha msukumo katika neva ambazo zimesambaa katika eneo hili la kichwa chako na hivyo kukusababishia kipandauso (Kichwa kuuma kupita kiasi) au hali ya kukosa raha.
2. Ujue kuwa wewe una gland mate (Saliva glands) zilizopo katika kinywa chako chote ambazo huchochea utengenezaji na utoaji wa mate wakati unapotafuta chingamu. Utoaji huu wa mate kwa hakika tunaweza kuuita kuwa ni matumizi mabaya ya nishati na rasilimali ambayo ingeweza kutumika kwa shughuli nyingi za umetaboli (Metabolic activities) katika kinywa.

4. Nyingi ya chingamu unazotafuna ni tamu, na hii imetokana na kupakwa kiambato kinachoitwa aspartame. Matumizi ya muda mrefu ya aspartame yanaweza kukusababishia kansa , kisukari , kuvurugika kwa mfumo wa ( Mfumo wa neva) na hitilafu wakati wa kujifungua. Na hata kama chingamu hiyo imepakwa tu sukari unaweza kupata matatizo kama hayo kwa kuanzia na mihemko isiyo ya kawaida.

3. La msingi hapa ni kuwa unapotafuna Chingamu ujue kuwa kuna hasara zake pia na hivyo jizuie kuifanya kuwa ndio kawaida yako ya maisha …itakugharimu!
(Kutoka vyanzo mbalimbali vya mitandao ya kiafya)

0 comments: