Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, January 20, 2011

Mwanamuziki lister Eliah , leo tulikuwa naye ndani ya studio za idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani-NHK World akitupa habari lukuki juu ya maisha yake ya kimuziki.Mwanamuziki huyu ana historia ya kusisimua sana .
Alianza kupiga piano akiwa na miaka mitano na baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari akajiunga na bendi ya King Kiki Double O ya Kikumbi Mwanza mpango Kiki, Sambulumaa, Bene Bene , Safari Sound Ochestra na baadaye M.K Group.Baadaye akajiendeleza Kimuziki huko Tanzania, nchini Austria na baadaye hapa Japani ambako sasa ameweka makazi yake.


Kukukumbusha tu wanaoujua wimbo original wa Sambulumaa Kadiri Kanshimba , kinanda kimepigwa na Lister.Tumeongea mengi na mwanamuziki huyu , hivyo ukitaka kumsikia kulia kwako kuna mitandao rafiki (Bofya NHK World) kisha angalia kipindi cha leo Alhamisi. Kwanza kuna habari zinzomuhusu mwalimu wa Iraq na ziara yake hapa Japani na baadaye mahojiano na Lister. Ilikuwa siku nzuri sana .Pata vionjo vya kinanda.

Pia unaweza kumpata kupitia mtandao wake wa : www.listerelia.com

Lister Eliah akiondoka mjengoni...

2 comments:

Anonymous said...

Shukran Bakari kwa mahojiano na huyu mkali wa Piano.Lister ni mwanamuziki wa kimataifa na ameshiriki katika matamasha mengi tu ya miziki ya Jazz akiiwakilisha nchi yetu.

Ni fursa nzuri kwa wanamuziki wengine kujifunza mbinu na njia zilizomfanya Lister afike alipo leo.

Vitabu alivyoandika vina mafunzo mengi kutuendeleza sisi ambao hatukupata nafasi ya kujifunza muziki shuleni.

Hongera Lister na endelea kutuwakilisha.

Mdau,Sweden.

Anonymous said...

Nimekuwa nikifuatilia kazi na maendeleo ya Lister tangu akiwa Benebene Group ambako alikuwa kiongozi wa bendi,akiwaongoza akina Carolla Kinasha,Athanas Lukindo,marehemu Dick Karashani,Chris Zondo,David Nhigula,Ali Msafiri na wengineo.
Nikaendelea kumfuatilia alipokwenda Sambulumaa na kurekodi nyimbo zote za kwanza kama Kadiri Kasimba(Kianga Songa RIP)Mama Happy(utunzi wake Lister),CCM imekua(Skassy Kasambula).
Nakumbuka kazi zake akiwa Safari Sound(Ndekule) pamoja na akina Mzee Muhidini,Kabeya Badu na wengineo kule Safari Resort Kimara.

MK Group(Ngoma za maghorofani pale New Africa na akina Joseph Mulenga- RIP,Mbombo wa Mbomboka,Kasongo Mpinda na wengineo.
Mpaka leo ninapoona kazi zake,kusema kweli amepiga hatua kubwa kimuziki/kiupigaji.
Naweza kusema jamaa yuko kwenye matawi ya juu na ni mfano wa kuigwa na wapiga vinanda wa kizazi kipya.
Asante Bakari kwa kutuletea kipindi ambacho kimetukumbusha mengi.
Ningependa kununua vitabu na CD zake,ningeshukuru kama ndugu Bakari unaweza kunisaidia mawasiliano na Lister.

JB,Singida Tanzania.