Wimbi la kutaka mabadiliko ya uongozi limetanda katika Ulimwengu wa Kiarabu likitokea Tunia, linavuma Misri, Lebanon, Yemen, albania na kuna fununu Libya!
Misri...
MISRI...
Moto wa kuung'oa utawala wa miaka 30 wa rais Hosni Mubarak nchini Misri umeshika kasi, wanajeshi wameingia mitaani baada ya wananchi kupambana na polisi na kuwafanya polisi waingie mitini, Rais Mubarak amevunja ukimya wake na kutangaza kulivunja baraza lake la mawaziri. Hali ni tete sana nchini Misri baada ya wananchi kujitokeza kwa wingi mitaani kuonyesha kuchoshwa kwao na utawala wa miaka 30 wa rais Hosni Mubarak."Utawala wa Mubarak huenda ukaangushwa wakati wowote kuanzia sasa, unasimama kwa mguu wake mmoja", alisema Mohamed ElBaradei mwanaharakati aliyezawadiwa tuzo ya amani ya Nobel ambaye amerudi Misri kuunga mkono maandamano ya kuung'oa utawala wa Mubarak.Mubarak kwa upande wake ameamua kuvunja ukimya wake kwa kulivunja baraza lake la mawaziri na kutangaza kuwa baraza jipya la mawaziri atalitangaza jumamosi.
Ijumaa ilikuwa ni siku ya nne ya maandamano ya kuung'oa utawala wa Mubarak ambapo maelfu ya watu walijiunga kwenye maandamano hayo baada ya sala ya ijumaa.Ili kupunguza nguvu ya waandamanaji ambao walikuwa wakitumia mitandao ya Twitter na facebook kuwasiliana, internet ilikatwa na makampuni ya simu za mikononi yalisitisha huduma za ujumbe wa simu.Polisi walirusha mabomu ya machozi na kuwashushia kipigo waandamanaji ambapo waandamanaji nao walijibu mapigo kwa kuyachoma moto magari ya polisi na kulichoma moto jengo la makao makuu ya chama tawala cha NDP.Magari ya wanajeshi yalipoingia mitaani majira ya jioni, waandamanaji hawakupambana na wanajeshi na badala yake waliyashangilia na kusalimiana na wanajeshi huku wengine wakiyaparamia magari hayo na kupata lifti za bure.
Jumla ya watu 18 wameishafariki hadi sasa wakati maandamano hayo yakijiandaa kuingia siku ya tano.Angalia VIDEO za maandamano hayo chini ikiwemo video ya jinsi kijana mmoja wa nchini humo alivyopigwa risasi na kuuliwa na polisi.
Albania....
Lebanon
Tunisia
Yemen:
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, January 29, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment