Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, February 18, 2011

JIJI la Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana alhamisi limejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya milipiko mikubwa ya mabomukutokea katika ghala namba tano la kutunzia silaha la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongolamboto, huku kukiwa na taarifa za watu 15 kufa na zaidi ya 60 kujeruhiwa. Nyumba nyumba kadhaa zikiteketea kwa moto baada ya kuangukiwa na mabomu.




Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi, alisema milipuko hiyo ilitokea ghala namba tano na kwamba, kilichokuwa kikifanyika ni kuzuia usienee sehemu nyingine.

Mwaka 2008 kulitokea mlipuko ghala la silaha kwenye kambi hiyo ya jeshi la Gongo la Mboto katika tukio ambalo vyombo vya usalama vilidai kuwa ulitokana na silaha hizo kupata joto kali.
Raisi jakaya Kikwete alitembelea eneo la tukio kujionea hali halisi na baadaye akaongea na waandishi wa habari..
Blogi ya MIRINDIMO inawapa pole wote waliofikwa na maafa haya , Mungu awape subra katika kipindi hiki kigumu wanachokabiliana nacho... (Picha kwa hisani kubwa ya Issa Michuzi Blog)

0 comments: