Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, February 18, 2011

Baada ya kusbiri kwa miaka mingi kuitwa baba Fulani hatimaye Ramajit Raghav amekuwa baba wa mtoto wa kiume kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 94 na ushee hivi.
Ramajit anayeishi katika kijiji kimoja nchini India anayefanya kazi katika shamba la kabaila mmoja nchini India kwa miaka 22 alimuoa Bi. Shakuntala, akiwa mke wake wa pili takriban miaka 10 iliyopita , mke ambaye sasa anasemekana ana miaka 50.
Bi. Shakuntala alilazwa katika hospitali ya Serikali katika mji wa Kharkoda na akajifungua kwa njia salama kabisa mtoto wake wa kiume.


Wazazi hao waliojawa na furaha tele walimuita mtoto wao jina la Karamjit na baba yake huyu alisema kuwa ilikuwa zawadi kutoka kwa Mwezi Mungu, na amempata mtoto huyo akiwa n fahamu zake na akili timamu.

Alipoulizwa juu ya maisha ya mtoto huyo kwa kuzingatia ukweli kuwa yeye ni mzee wa miaka 94 , Mzee Rajamit alisema kuwa “ najua hakuna baya litakalotokea kwa mtoto wangu , Mye nitakufa tu ikiwa nyoka mweusi atanigonga na hiyo haitokei leo wala kesho”. Mzee huyo hakuishia hapo akasema “Nitembelee tena baada ya miaka 10 utanikuta kama unavyoniona hii leo”.
Kuzaliwa kwa mtoto huyu kunamfanya Ramajit kuvunja rekodi ya mzazi wa zamani aliye na umri mkubwa zaidi ambaye alipata mtoto akiwa na miaka 90 akiwa amepata mtoto wake wa 22 mwaka 2007 na huyu ni Nanu Ram Jogi, -
(Habari hizi ni kwa mujibu wa Shirika la habari la ATULA la huko India).

0 comments: